Ronaldo achechemea katika mazoezi

Image caption Ronaldo

Mshambuliaji wa kilabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo alichechemea na kutoka nje dakika chache kabla ya kukamilika kwa mazoezi siku ya Jumanne,na hivyobasi kuzua uvumi kuhusu uzima wake kwa kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Mchezaji huyo bora aliyewahi kushinda taji la Ballon d'Or anauguza jeraha la paja ambalo lilimlazimu kukosa mechi tatu mnamo mwezi Aprili.

Image caption Ronaldo

Alitoka nje baada ya kipindi cha kwanza cha mechi ya mwisho ya la Liga.

Real Madrid itakabiliana na Atletico Madrid mjini Milan wikendi hii katika marudio ya mechi ya fainali ya 2014 ambapo Real iliibuka mshindi.

Image caption Ronaldo

Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 31,amefunga mabao 51 kwa Real Madrid msimu huu.