Mwanasoka bora wa BBC: Kim Little

Haki miliki ya picha Getty
Image caption mwansoka bora mwaka wa BBC upande wa Wanawake kwa mara ya pili Kim Little

Kiungo wa timu ya soka ya Scotland Kim Little, ameshinda tuzo ya pili ya mwansoka bora mwaka wa BBC upande wa Wanawake

Kim Little, mwenye umri wa miaka ishirini na mitano ambaye anachezea klabu ya Seattle Reign iliyoko nchini Marekani, aliibuka kileleni kwa kura nyingi zilizopigwa na washabiki zake.

Kim aliwapiku wachezaji wengine bora walioteuliwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho cha kuwania tuzo hiyo kutoka katika nchi za Cameroon,Ufaransa na Marekani.

Naye kocha wa timu ya Scotland, Anna Signeul amesema kwamba anakiri kuwa ushindi wa Kim umekuwa wa ajabu kidogo, ambaye anamuelezea Kim kama mchezaji aliyejaaliwa kila kitu ,ikiwemo kasi, mwenye mizania na mwenye kipaji na mbinu za hali ya juu mchezoni.