Paul Scholes: Mourinho ndio dawa ya Man United

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa mchezaji wa Man United Paul Scholes

Jose Mourinho atajifunza kutoka kwa uzoefu wa Louis van Gaal na kuimarisha mchezo wa klabu ya Manchester United iwapo atachaguliwa kuwa mkufunzi wa timu hiyo.

Mazungumzo ya kumleta Mourinho katika uwanja wa Old Trafford yameingia siku yake ya pili.

Van Gaal alifutwa kazi siku ya Jumatatu ,siku mbili tu baada ya kushinda kombe la FA.

''Mashabiki katika klabu ya Man United wanahitaji mchezo wa kufurahisha na nina hakika Mourinho atakuja na kuisadia Man United'',alisema aliyekuwa kiungo wa kati wa timu hiyo paul Scholes.

Van Gaal aliiongoza United hadi nafasi ya tano katika ligi ya Uingereza lakini alikosolewa kwa mchezo wake usio na mashambulizi huku timu hiyo ikifunga mabao 49 msimu huu.