Serengeti boys wamaliza nafasi ya tatu

Image caption Serengeti Boys

Timu ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys imemaliza katika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya vijana yaliyofanyika huko Goa nchini India.

Serengeti boys walishinda mchezo Wa mwisho dhidi ya Malaysia kwa 3-0 maboa ya vijana wa timu hiyo yalifungwa na Rashid Abdallah, , Shabani Zuberi, na Muhsini Malima,

AIFF Youth Cup ni Mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la India, All India Football Federation mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya Mashindano ya yanayowakabili.

Michuano hii imetumika kuwapa vijana na timu ya Serengeti mazoezi kujianda na mchezo wao wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Africa dhidi ya Shelisheli .