Arsenal yamsajili Granit Xhaka

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Granit Xhaka

Klabu ya Arsenal imemsajili kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Switzerland Granit Xhaka kutoka klabu ya Borussia Monchengladbach.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23,ambaye amecheza kimataifa mara 41 na kuwa nahodha wa klabu hiyo ya Ujerumani anajiunga na Arsenal kwa kiasi cha pauni milioni 35 katika kandarasi ya mda mrefu.

''Nafurahia kujiunga na Arsenal'',alisema Xhaka.''Nataka kuhamia mjini London ili kuiwakilisha kilabu hii na kucheza katika ligi ya Uingereza''.

''Nitafanya kila kitu kuwapatia taji Arsenal na kuwafurahisha mashabiki''.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alisema: Granit Xhaka ni mchezaji mzuri aliye na uzoefu wa michuano ya vilabu bingwa Ulaya na ile ya Bundesliga.

''Tumekuwa tukimfuatilia kwa mda mrefu na ni mchezaji atakayeongeza maarifa katika kikosi chetu''.