Rafael Benitez kusalia Newcastle

Image caption Rafael Benitez

Rafael benitez ameamua kusalia katika klabu ya Newcastle baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka mitatu kufuatia kushushwa daraja kwa timu hiyo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 na raia wa Uhispania aliajiriwa mnamo mwezi Machi kufuatia kufutwa kazi kwa Steve Mc Claren lakini akashindwa kuinusuru timu hiyo kushushwa ngazi.

Katika kandarasi yake alikuwa na fursa ya kuondoka iwapo Newcastle ingeshushwa daraja na wengi walitarajia angefanya hivyo.

''Upendo niliosikia kutoka kwa mashabiki ulikuwa ushawishi mkubwa'',alisema.

Kocha huyo aliyewahi kuifunza ,Liverpool,Chelsea na Real Madrid atachukua udhibiti wa maswala yote yanayohusisha kandanda katika kilabu hiyo,Newcastle imesema.