Alexander Gauland adaiwa kutoa matamshi ya kibaguzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jerome Boateng adaiwa kutolewa matamshi ya kibaguzi

Naibu kiongozi wa Chama cha kupambana na uhamiaji nchini Ujerumani amezungumza maneno ya kibaguzi dhidi ya mchezaji nyota wa Ujerumani Jerome Boateng ambaye baba yake ni raia kutoka Ghana.

Alexander Gauland,aliliambia Gazeti la Ujerumani la (the Frankfurter Allgemeine) kuwa watu wanafikiri Boateng ni mchezaji mzuri lakini kamwe hatomuhitaji kama rafiki yake.

Gauland alilaaniwa vikali na wachezaji mbalimbali,Waziri wa mambo ya ndani pamoja na Rais wa shirikisho la soka nchini Ujerumani ,Reinhard Grindel amesema maneno yake kuwa hayana maana.

Gauland baadaye alijibu kuwa hakumaanisha kumdhalilisha Jerome Boateng ambaye amekuwa nguzo muhimu kwa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani.