Mchezaji wa Mexico aliyetekwa nyara aokolewa

Image caption Alan Pulido

Walinda usalama nchini Mexico wamemuokoa mchezaji nyota wa soka anayesakata dimba la kulipwa nje ya nchi, Alan Pulido, aliyetekwa nyara mwishoni mwa juma.

Maafisa wanasema kuwa anakaguliwa kimatibabu.

Mchezaji huyo amewaonyesha wanahabari mkono uliofungwa na maafisa wa matibabu baada ya kuumizwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alan Pulido

Mwanasoka huyo anayeichezea timu ya Ugiriki ya Olympiakos, alitekwa nyara katika mji anakotoka wa Ciudad Victoria ulioko kaskazini mwa jimbo la Tamaulipas.

Maafisa wa eneo hilo wanasema kuwa aliokolewa muda mfupi kabla ya usiku wa manane kuamkia leo asubuhi lakini hawakutoa taarifa za operesheni ya walinda usalama ya namna ilivyotekelezwa.

Maelfu ya watu hutekwa nyara nchini Mexico kila mwaka, mara nyingi na magenge yanayohusika na ulanguzi wa dawa za kulevya