Serge Aurier aongezewa muda wa kizuizini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serge Aurier

Polisi wa Ufaransa wameongeza muda wa saa 24 ya kukaa kizuizini kwa mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Serge Aurier, huko Paris, ili kutoa nafasi zaidi ya uchunguzi .

Aurier mwenye umri wa miaka 23 , ambaye huchezea timu ya Paris ya PSG anadaiwa kuwa na mabishano na polisi.

Hapo awali alikuwa amekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi mapema Jumatatu baada ya kisa hicho huko Paris.

Mchezaji huyo anadaiwa kumpiga polisi mmoja katika koo yake.

Kisa hicho kilitokea eneo la Champs Elysee katika majira ya asubuhi ambapo Aurier alikuwa akitoka kilabuni.