Mwingine akamatwa utekaji wa Pulido

Image caption Alan Pulido,mwanasoka aliyetekwa nyara

Polisi nchini Mexico katika jimbo la Tamaulipas wamemkamata mtu wa pili aliyehusika kwenye utekaji wa mwanasoka Alan Pulido mwisho wa juma lililopita.

Mshukiwa Osvaldo Garcia amemuoa binamu wa mchezaji huyo ndiye anayetuhumiwa kuongoza utekaji nyara huo. Aliwekwa kizuizini baada ya kurushiana risasi na polisi mjini Ciudad Victoria.

Watekaji walihitaji kiasi cha pesa ili Pulido aweze kuachiliwa lakini mwanasoka huyo aliweza kuwashinda nguvu na kuwapigia polisi,waliomuokoa na mtekaji mmoja kukamatwa.