Dani Alves kuondoka Barcelona

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dani Alves

Beki wa kulia wa Brazil Dani Alves anaondoka Barcelona, kulingana na klabu hiyo.

Alves mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na Seveilla mwaka 2008 na kushinda mataji 3 ya ligi ya vilabu bingwa pamoja na mataji sita ya La Liga na Barcelona.

Mkurugenzi wa Barca Robert Fernandez aliambia mtandao wa twitter wa kiabu hiyo : Dani Alves ameamua kuondoka.

''Ni uamuzi wa kibinafsi ambao tunauheshimu''.

Alves pia alishinda kombe la Copa del Rey mara nne na Braca ambao walishinda taji la ligi na kombe msimu huu.