Manchester City yamsajili Gundogan

Image caption Mchezaji IIKay Gundogan kutoka klabu ya Borussia Dortmund

Klabu ya Manchester City imemsajili kiungo wa kati wa Ujerumani IIkay Gundogan kutoka kwa kilabu ya Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka minne.

Mchezaji huyo wa miaka 25 ambaye hatoshiriki katika michuano ya Euro 2016 pamoja na kuanza kwa ligi ya Uingereza msimu huu kutokana na jeraha atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa kilabu ya Mancity Pep Guardiola.

Manchester City imeripoti kulipa kitita cha pauni milioni 20 kumpata Gundogan.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Pep Guardiola

''Nilipogundua kwamba City walikuwa wakinihitaji,moyo wangu ulikubali'',alsiema.''Mambo yamenda haraka sana''.

Mkurugnzi wa klabu hiyo ya Ligi ya Uingereza Txiki Begiristain alipongeza maadili ya Gundogan pamoja na uwezo wake