Euro: Uingereza yaishinda Ureno

Haki miliki ya picha PA
Image caption Chris Smalling,mlinzi wa kati wa Uingereza

Uingereza wamekamlisha maandalizi yao ya Euro 2016 kwa ushindi mwembamba dhidi ya Ureno iliyocheza ikiwa na watu kumi katika dimba la Wembley.

Chris Smalling alimalizia kwa kichwa mpira uliopigwa na Raheem Sterling aliyeingia kutoka benchi na kuandika bao hilo la pekee. Timu ya Ureno ilicheza pungufu kutokana na mlinzi wake wa kati Bruno Alves kuonyeshwa kadi nyekudu baada ya kumchezea madhambi mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane dakika ya 35. Jambo pekee la kufurahisha kwa Hodgson ni kwamba wachezaji wake wote wapo tiyari kiafya kushiriki michuano ya Euro 2016.