Jamie Vardy kutua Arsenal ?

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jamie Vardy

Kijana wa miaka 29 Jamie Vardy kutoka Leicister City anatarajiwa hii leo kutoa majibu iwapo atajiunga na Club ya Arsenal kabla hajaelekea kwenye michuano ya Euro za mwaka huu akiwa na timu ya taifa la Uingereza.Arsenal tayari wamefikia makubaliano na Leicester na wamemwekea mezani Vardy kitita cha fedha kwa miaka minne.

Vardy bado alikuwa anatafakari kama awaache Mbweha kuelekea kwa washika Bunduki. Itakumbukwa Vardy aliisaidia sana Leicister katika kutwaa taji la Ligi kuu akifunga mabao 24.