Rio2016: Wanariadha wakimbizi wafanya mazoezi Kenya

Image caption Wanariadha wakimbizi watakaoshiriki Olimpiki

Wanariadha wakimbizi kutoka kote duniani wamekuwa wakifanya mazoezi kwa bidii, lengo kuu, kushiriki katika michezo ya Olympic chini ya bendera ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki.

Katika viungani mwa jiji la Nairobi, ni wakfu wa Tegla Loroupe, ambao unasimamia mazoezi ya wanariadha watano kati ya kumi waliochaguliwa kushiriki Michezo ya Olmpiki kule Rio de Janeiro, Brazil.

Tegla Lorupe, anashikilia rekodi kadhaa za mbio duniani na alikuwa mwanamke wa kwamza kutoka Afrika kushinda mbio za nyika za New York City, alianzisha wakfu huu na nia za kuinua talanta kutoka maeneo ambayo yanakumbwa na vita na dhamira ya kudumisha amani.

Alifanikiwa kuzuru kambi za wakimbizi kaskazini mwa kenya na kuweza kutambua wasichana kwa wanaume ambao wanaweza kukimbia, aliwaleta Nairobi na kuwapea wakufunzi wa kuhakikisha kwamba wamejiandaa vilivyo.

Mbona msukumo huu, Tegla anasema, "kama mwanariadha, nilifahamu kwamba kuna mengi ambayo ninaweza kufanya kando na kushiriki mashindano Ulaya na kuishi vizuri.

Image caption Tecla Lorupe

watu ambao wamefaulu huwa wanasahau nyumbani, lakini mimi sikusahau nyumbani, nilirudi na kuanza mashindano ya kuleta amani na mimi kuwaona hawa wanariadha wakienda Rio kwa ajili ya amani ninafurahia"

Mmoja wa wale ambao walifuzu ni Angelina Naidai. Ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini mwenye umri wa miaka 22, alitoroka vita kutoka Sudan kusini akiwa na miaka minane tu, na hajawahi kuona familia yake tena.

Wazo la kuwahi kuona familia yake ndilo linampa msukumo, anasema.

"Nitakapoenda, lazima nirudi kama mtu wa maana, mtu tofauti, ndiposa niweze kuenda kutafuta familia yangu, kwa sasa hata siwajui, siwezi kuwatambua hata, labda wanafananishe na jamii yangu ambao nafanana nao".

Na kwa wale ambao hawakufaulu, wamepata kuona nuru katika maisha ya baadaye ya kukombolewa katika minyororo ya ukimbizi.

Image caption Wanariadha wakimbizi watakaoshiriki katika michezo ya Olimpiki

Riek Thiep, mwenye Umri wa miaka 24, pia ni mkimbizi kutoka sudan kusini, alishuhudia mauaji ya mama na dada yake, na kutoroka sudan Kusini, alijipata katika kambi ya waimbizi ya Kakuma kaskazini mwa Kenya, na akajitahidi hadi hapa Nairobi na lengo la Kuwa bingwa siku moja.

"Siku moja, wakati mmoja, nitakua mtu wa maana, olimpiki za 2012, raia wa Uganda alishinda medali ya dhahabu, alinifurahisha sana hasa alayokuwa akizumgumza, alisema ata akifa yeye ni Bingwa, kwa hiyvo siku moja watu watasema alikuwa bingwa wa medali ya dhahabu katika Olimpiki,” anasema.

Mada zinazohusiana