Rio2016: Je,wayajua majukumu mengine ya wanariadha wa Kenya?

Image caption David Rudisha

Uwanjani wanariadha wa Kenya wamekuwa wakililetea taifa hilo medali, lakini unafahamu kuwa wanariadha hao hutumia mda wao mwingine kulihudumia taifa la Kenya?

Kikosi cha Kenya kitakachoshiriki rio, kitawajumuisha wanariadha, ambao mbali na uanamichezo, ni watumishi wa umma nchini Kenya.

Wanariadha, David Rudisha, Jemima Sumgong, Julius Yego na Ezekiel Kemboi, ni miongoni mwa wawakilishi wa Kenya rio watakaovaa sare za wanariadha mbali na sare za askari.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ezekiel Kemboi

Rais Uhuru Kenyatta, akiikabidhi timu ya Kenya ya olimpiki bendera, aliwashangaza wengi alipotoa wito kwa Ezekiel Kemboi na kumuita 'mlinzi wangu, na wengi walishangaa kwani hawakufahamu alikuwa mlinzi wa Rais.

'Huyu ni askari wangu, Bwana Kemboi,'' Nawatakia kila la heri. alisema.

Miongoni mwa maafisa wa Polisi watakaoiwakilisha Kenya ni David Rudisha, Ezekiel Kemboi, Asbel Kiprop, Geoffrey Kamworor, bingwa mbio za mita elfu kumi, 10000m, Vivian Cheruiyot, na Eunice Sum. Hali kadhalika, Kenya itawakilishwa kwenye mbio za 3000m kuruka viunzi na maji na afisa wa polisi Hyvin Kiyeng.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Asbel Kiprop

Nahodha wa timu ya Kenya ya Olimpiki. Wesley Korir, ni mbunge aliyechaguliwa katika uchaguzi wa mwaka wa 2013.

Korir amekuwa akiishinikiza bunge la Kenya lipitishe ule mswada ambao sasa ni sheria juu ya udhibiti wa dawa zilizoharamishwa kwenye michezo.

Juhudi zake zilichangia kuliwezesha bunge kuandaa vikao maalum kujadili na kupitisha mswada huo ili kuzuia Kenya kupigwa marufuku ya kutoshiriki Olimpiki.

Je, ni vipi wanaendesha kazi zote?

Image caption Vivian Cheruiyot

''Ni kujipanga na kufanya kinachostahili wakati ufaao, alisema Ezekiel Kemboi, bingwa wa dunia mbio za mita 3000,''.

Aidha afisa wengine wa idara ya ulinzi nchini Kenya, ni mwakilishi katika mbio za mita 200, Mike Mukamba, Katika kitengo cha kutembea, kilomita 20km Samuel Gathimba, kwenye mbio za mita 400, Alphas Kishoyan, mwanajeshi atakuwa akisaka medali na mwenzake Boniface Mweresa.

Kwa upande wa wanawake, Kenya itawakilishwa na maafisa kama vile, mkimbiaji wa mbio za mita elfu tano, Helen Obiri na mwanariadha Grace Wanjiru, mshiriki wa kitengo cha kutembea, kilomita 20.

Image caption Wanariadha wa Kenya

Mwanariadha mstaafu na mshindi wa medali ya fedha katika Olimpiki 2004 na 2008, Catherine Ndereba ni mmoja wa maafisa wakuu katika idara ya magereza nchini Kenya.

''Ni vyema kuiwakilisha nchi na pia kufanya kazi vyema, sio kazi rahisi lakini inahitaji bidii,'' alisema.

Wanariadha hawa wamekuwa wakijinoa katika mbio za kila mwaka kwa idara za maafisa wa polisi na kijeshi nchini Kenya.

Mada zinazohusiana