Man City yaomba kusajili kipa wa muda

Manchester City imeiandikia Bodi ya Ligi Kuu ya England ikiomba iruhusiwe isajili mlinda mlango kwa mkopo wa dharura hadi msimu huu utakapomalizika. BBC imegundua kuwa Bodi ya Ligi Kuu ya England huenda ikatoa idhini kwa City kusajili mlinda mlango wa muda kuziba pengo la mlinda mlango wao Shay Given aliyeumia.

Shay Given hataweza kucheza katika michezo mitatu iliyosalia kabla ligi haijamalizika baada ya bega lake kuchomoka siku ya Jumamosi walipotoka sare ya kutofungana na Arsenal.

Stuart Taylor ambaye ni mlinda mlango wa akiba naye hali yake si nzuri,