McCarthy kukosa fainali za kombe la dunia

kombe la dunia
Image caption kombe la dunia

Mshambulizi matata wa Afrika Kusini ambaye anaongoza kwa idadi ya ufungaji wa mabao, Benni McCarthy ameachwa nje ya kikosi kitakachoakilisha nchi hiyo kwenye fainali za kombe la dunia zitakazo anza siku 10 zijazo nchini Afrika Kusini.

Mchezaji huyo anayechezea klabu ya West Ham hajaonyesha mchezo mzuri katika miezi ya hivi karibuni na kuwa ameshutumiwa kwa kuongeza uzani.

McCarthy ni miongoni mwa wachezaji waliochujwa kutoka kwa orodha ya awali ya wachezaji 28 waliokuwa kambini wakijiandaa kwa fainali hizo.

Wengine waliotemwa ni pamoja na mlinda lango Rowen Fernandez, Bryce Moon, Innocent Mdledle na mchezaji wa kiungo cha kati Franklin Cale.

Kikosi kamili cha Afrika Kusini ni kama ifuatavyo:

Itumeleng Khune (Kaizer Chiefs), Moeneeb Josephs (Orlando Pirates),Shuaib Walters (Maritzburg United); Siboniso Gaxa (Sundowns), Anele Ngcongca (Genk), Aaron Mokoena (Portsmouth), Matthew Booth (Sundowns), Bongani Khumalo (SuperSport United), Siyabonga Sangweni (Golden Arrows), Tsepo Masilela (maccabi Haifa), Lucas Thwala (Orlando Pirates); Teko Modise (Orlando Pirates), Lance Davids (Ajax Cape Town), Reneilwe Letsholonyane (Kaizer Chiefs), MacBeth Sibaya (Rubin Kazan), Thanduyise Khuboni (Golden Arrows), Kagiso Dikgacoi (Fulham), Steven Pienaar (Everton), Siphiwe Tshabalala (Kaizer Chiefs); Surprise Moriri (Sundowns), Bernard Parker (FC Twente), Katlego Mphela (Sundowns), Siyabonga Nomvethe (Moroka Swallows)