Liverpool yasema "La hasha!"

Goli la Kuyt laiwezesha Liverpool kutoka sare
Image caption Dirk Kuyt

Bao la Dirk Kuyt kupitia mkwaju wa penalti liliiwezesha timu yake ya Liverpool kutoka sare ya 2-2 ilipocheza na jirani zao Everton.

Licha ya Liverpool kucheza katika uwanja wa nyumbani wa Anfield, sare hiyo inazifanya timu hizo kuvuka msitari wa kushuka hadhi kwa pointi nne tu.

Raul Meireles alifanikiwa katika kupata bao la kwanza katika mechi hiyo, kwa mkwaju kutoka yadi 18.

Awali kipa Tim Howard alikuwa ameiokoa Everton kutoka mikwaju miwili ya Kuyt.

Everton iliweza kusawazisha kupitia bao la kichwa la Sylvain Distin, kabla ya Jermain Beckford kuweza kuwafanya kuongoza, kwa kupata bao la pili.

Lakini wakati mlinda lango Howard alipomtega Maxi Rodriguez, Kuyt aliweza kufunga goli la penalti.

But when Howard tripped Maxi Rodriguez in the box, Kuyt fired in to level.

Kufuatia Kenny Dalglish kuwa kuchukua madaraka ya meneja katika uwanja wa Anfield baada ya miaka 20, mashabiki walikuwa wanatazamia Liverpool kung'ara katika mechi hiyo, na kabla ya mechi, waliimba wimbo wao maarufu kwa bidii "You'll never Walk Alone", yaani hautetembea ukiwa mwenyewe katika hali ya upweke, wakitazamia ushindi.

Licha ya meneja Roy Hodgson kutimuliwa, mpango wa Dalglish haujakwenda kwa taratibu, kwani Liverpool ilishindwa na Manchester United katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA, na vile vile kuchapwa na Blackpool katika ligi kuu ya Premier.