FIFA tayari kuisikiliza rufaa

Wajumbe wa kamati kuu wa shirikisho la kimataifa FIFA, Amos Adamu na Reynald Temarii, rasmi wamekata rufaa kwa kusitishwa katika kazi zao, kufuatia madai ya ufisadi.

Image caption Wajumbe wote wawili wamekanusha makosa dhidi yao

Adamu kutoka Nigeria alisitishwa kazi kwa muda wa miaka mitatu, baada ya waandishi kumwekea mtego, wakiwa na nia ya kuonyesha alikuwa tayari kupokea hongo.

Temarii, kutoka Tahiti, aliepuka lawama za ufisadi, lakini akasitishwa kazi kwa mwaka mmoja, kwa kuvunja kanuni za utendaji kazi za shirikisho la FIFA.

Wote wanadai hawana makosa, na shirikisho la FIFA sasa litaisikiliza rufaa yao tarehe 2-3 mwezi ujao wa Februari.