Lord Coe aunga mkono West Ham

Mwenyekiti wa kamati ya michezo ya Olimpiki ya London 2012, Lord Coe, anaamini kuwa wana wajibu wa kuhifadhi uwanja wa Olimpiki kuwa uwanja wa riadha na michezo tofauti.

Image caption Uwanja wa Olimpiki

Tottenham na West Ham wanataka kuumiliki uwanja huo na Tottenham wanataka kuondoa sehemu ya riadha.

'Ni jambo lenye uzito na ni lazima tuzitimize ahadi zetu ikiwa hatungependa kujiharibia jina letu, na kupoteza heshima,' alisema.

'Itakuwa vigumu sana kuheshimiwa katika jamii ya wanamichezo au popote pale.'

Uamuzi kuhusu mustakabali wa Uwanja wa Olimpiki inatarajiwa Ijumaa.

West Ham wanaowania kuimiliki uwanja huo wanaungwa mkono na halmashauri ya eneo hilo.

Iwapo wataumiliki uwanja huo watukuwa wamehama maili mbili kutoka uwanja wao wa Upton Park na wangependa kuufanyia ukarabati bila kuondoa sehemu ya riadha.

Tottenham nao watahama urefu wa maili tano kutoka White Hart Lane na pendekezo lao ni kuondoa sehemu ya riadha na kuuufanya kuwa uwanja wa soka.