Orient yaikwaza Arsenal

Manchester United kukutana na mshindi kati ya Arsenal na Leyton Orient katika mechi ya marudiano baada ya Orient kusawazisha mnamo dakika ya 89.

Rosicky alikuwa ameipatia Arsen al bao lake la kwanza katika kipindi cha pili lakini Jonathan Tehoue aliyeeingia mda mfupi kabla akapangua mipango ya Arsene Wenger kwa kufunga bao la kusawazisha mnamo dakika ya mwisho.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Arsena au Orientl kukutana na Man U

Hivyo basi Arsenal itabidi ipambane tena na Leyton Orient kwenye uwanja wa Emirates kabla ya kuingia robo fainali za Kombe la FA ambapo mshindi atakutana na hasimu wa Arsenal, Manchester United.

Manchester City, au Aston Villa, watakuwa ni wenyeji wa Everton au Reading, huku Stoke nao watakuwa nyumbani kuikaribisha West Ham or Burnley.

Katika pambano la vilabu viwili vya ligi ya Premier, Bolton itasafiri kucheza na Birmingham.

Mechi za robo fainali zitachezwa kati ya tarehe 12 hadi 13 Machi.

Manchester United, ambao wanaongoza katika ligi kuu ya Premier, jana waliweza kupenya kwa kuifunga timu ambayo haimo katika michuano ya ligi, Crawley, bao 1-0, katika mechi ya raundi ya tano.

Mara ya mwisho Man U kukutana na Arsenal katika Kombe la FA ilikuwa ni mwaka 2008, wakati Man U ilipopata ushindi wa magoli 4-0.

Awali timu ya Arsene Wenger iliweza kuiangusha Man U mwaka 2005 kupitia mikwaju ya penalti.

Mabingwa watetezi Chelsea walishindwa na Everton kupitia mikwaju ya penalti katika mechi iliyocheza Jumamosi.

Droo ya robo fainali

Stoke v West Ham au Burnley Man City au Aston Villa v Everton au Reading Birmingham v Bolton Manchester United v Leyton Orient au Arsenal