Walcott kukosa fainali

Theo Walcott
Image caption Aliondolewa kwa machela katika mechi dhidi ya Stoke

Mchezaji wa Arsenal, Theo Walcott, hataweza kupambana katika mechi ya fainali, Kombe la Carling dhidi ya Birmingham, siku ya Jumapili, baada ya kujeruhiwa katika mechi dhidi ya Stoke, na ambayo timu yake ilipata ushindi wa goli 1-0.

Walcott aliumia kifundo cha mguu wa kushoto, baada ya kung'anga'nia mpia na Dean Whitehead, na ilibidi aondolewe uwanjani kwa machela.

"Ameteguka kifundo cha mguu, na ni wazi kwamba hataweza kucheza katika mechi ijayo", alieleza meneja Arsene Wenger.

Wenger alisema nahodha Cesc Fabregas naye atachunguzwa pia kuthibitisha kama alijeruhiwa vibaya kuliko inavyofikiriwa katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.