Dalglish apata mkataba mpya

Kenny Dalglish ametia saini mkataba wa miaka mitatu kuwa meneja wa klabu ya Liverpool ya Uingereza.

Mshambulizi huyo wa zamani kutoka Uskochi, alikubali tena kwa mara ya pili kuifundisha Liverpool, alipochukua madaraka ya Roy Hodgson, ambaye alitimuliwa mwezi Januari.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kuifundisha Liverpool kwa miaka 3

Tangu kuanza kazi hiyo yake mpya klabu kimefanikiwa kuimarisha matokeo yake.

Klabu hiyo ya kaskazini-magharibi mwa Uingereza sasa inashikilia nafasi ya tano katika ligi kuu ya Premier, na ikiwa inakaribia kujiandikishia nafasi ya kufuzu kwa mashindano ya ligi ya Europa msimu ujao.

Leo Alhamisi Dalglish amesema; "Nilipoikubali kazi hii mwezi January, nilisema mimi nitafurahi katika kuisaidia klabu msimu uliosalia....sasa wanaomiliki klabu, katika busara yao wameamua nisalie kwa muda mrefu zaidi".

Kocha msaidizi, Steve Clarke, naye vile vile amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitatu, kuwafundisha mabingwa hao wa ligi kuu mara 18.