Tevez akashifu Manchester

Nahodha wa Manchester city Carlos Tevez amesema kuwa mmiliki wa klabu hiyo, Sheikh Mansour, amemruhusu kuondoka akitaka.

Image caption Sheikh Mansour

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwasilisha ombi la kuhama klabu hiyo katikati ya msimu uliopita kinyume na habari za kukanusha taarifa hizo.

Tevez alisema kuwa angependa kuihama Uingereza na kuwa karibu na familia yake.

Nahodha huyo aliyepewa fursa ya kipekee kwa kuongezewa kitita cha kishindo baada ya klabu hiyo kushinda Kombe la FA, amesema katika mahojiano na jarida la News of the World kwamba Sheikh Mansour ametumia kila njia na mbinu asiondoke, na endapo nitakaa huko itakuwa na kwa sababu yake.

Tevez aliongezea kua ni yeye aliyenisajili na angependa niichezee klabu yake na wakati huo huo kuniambia nipo huru kufanya linaloniridhisha.

Aliniongezea mkataba mpya mwezi disemba lakini sitaki kuongezea mda wangu huko MANCHESTER.

Mwisho wa msimu nikaombwa nitie saini mkataba mpya na sina hakika kama nitakubali.

Image caption Carlos Tevez

Licha ya kuishi mjini Manchester kwa takriban miaka minne,Tevez hana mapenzi na mji huo.

Akizungumza na kituo cha Televisheni ''Telefe'' cha huko Argentina alikariri msimamo wake na jinsi anavyochukizwa na maisha mjini Manchester.

Alisema "hakuna lolote katika mji wa Manchester. Tatizo ni kuwa bado kiingereza kinanipa tabu. Mkataba wangu utakapomalizika sitorudi huko wala sitaki kuusikia, yaani hata nikitaka kwenda mapumziko siwezi kutembelea Manchester daima abadan"

Bado haijaeleweka kama kauli hiyo ya Tevez utakuwa ndiyo mwisho wa Tevez kuichezea klabu hiyo au atarudi kukamilisha mkataba wake hadi mwisho.