Gullit atimuliwa na Terez ya Chechnya

Habari kutoka Ligi ya Chechnya zinasema kuwa Kocha wa klabu ya Ligi kuu Terek Grozny, Ruud Gullit amefutwa kazi baada ya timu yake kufungwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mchuano kati ya Terez na Lokomotif Moskow

Gullit aliteuliwa kuiongoza klabu hiyo ya Chechnya mnamo mwezi januari lakini alionywa na Rais wa klabu hiyo Ramzan Kadyrova kuwa lazima Terek ishinde mechi dhidi ya Amkar Perm hii leo.

Kufuatia kipigo cha 1-0 , Kadyrov aliliambia shirika la habari la Interfax kuwa "Gullit hatoifunza tena Terek. Chini ya uongozi wake Timu imeshindwa kupiga hatua ."

Rais wa klabu hio amenukuliwa akisema kuwa Gullit amesababisha klabu kushuka hadi nafasi ya 14 kati ya vilabu 16 vya Ligi hiyo.

Gullit mwenyewe amesema kuwa hadhani kama ushindi ungebadili lolote. Ni mpango uliokuwepo kuipoteza kazi hiyo" Itakumbukwa kuwa Ruud Gullit aliwahi kuwa mkufunzi wa Chelsea, Newcastle, Feyenoord na LA Galaxy ya Marekani.

Alipowasili Chechnya alipewa jukumu la kuikwamua Terek kutoka ilikokuwa hadi angalau nafasi ya nane lakini ushindi wa mara tatu katika mechi 13 haukutosha kuikwamua na kuiacha ikikaribia mkasi wa kudondoshwa mwishoni mwa msimu.