Bayern yamtaka Alex kutoka Chelsea

Bayern Munich imeingiwa tamaa ya kumsajili beki wa Chelsea, Alex BBC imefahamishwa.

Klabu hiyo ya Ligi ya Bundesliga imebadili muelekeo baada ya juhudi zake kumsajili Jerome Boateng wa Manchester City kushindikana kutokana na klabu yake kuomba kiwango kikubwa kabla ya kumuacha ahamie Ujerumani.

Image caption Bayetn munich

Branislav Ivanovic atabeba zigo la majukumu akiondoka Alex, na kutegemea wenzake John Terry na David Luiz kama mabeki wenye uzowefu Klabu ya Chelsea.

Chelsea yenyewe haijaingia sokoni kwa usajili wa majira ya joto ikikumbukwa kuwa ilitumia pauni milioni 71 katika dirisha la januari kuwasajili Luiz na mshambuliaji Fernando Torres.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alex kushoto

Hadi sasa Chelsea imekataa kujibu lolote kuhusu ripoti kuhusu Alex.

Tangu mwisho wa msimu uliopita wachezaji watatu wameihama klabu hiyo na kujiunga na Hamburg huko Ujerumani- Michael Mancienne, Jacopo Sala na Gokhan Tore.

Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa michezo wa klabu ya Chelsea Frank Arnesen, ambaye sasa ndiye mhusika mkuu wa masuala ya usajili, imearifiwa kuwa anakaribia kumsajili beki wmwingine wa Chelsea Jeffrey Bruma kwa mkopo wa kipindi cha miaka miwili.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Frank Arnesen

Chelsea kwa wakati huu haina Meneja baada ya kumfukuza Carlo Ancelotti , kufuatia msimu uliomalizika bila lolote kwa mara ya kwanza katika Misimu mitatu.

Alex alijiunga na Chelsea uwanja wa Stamford Bridge mnamo mwaka 2004 lakini ikabidi akopwe PSV Eindhoven kwa sababu hakuwa na uzowefu wa kutosha na hajashiriki mechi za kutosha na Timu ya Taifa lake Brazil kukubalika kwa utaratibu wa England.