Spurs haitamuuza Modric

Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Tottenham Hotspur inayocheza katika ligi kuu ya Premier ya England, Daniel Levy, amesema klabu hakina nia ya kumuuza Luka Modric kwa "bei yoyote ile".

Kiungo cha kati Modric, kutoka Croatia, ameonyesha nia ya kutaka kujiunga na wapinzani Chelsea, pia katika ligi kuu ya Premier.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Anataka kujiunga na Chelsea pasipo kuwaudhi Spurs

Chelsea wako tayari kutoa kitita cha pauni milioni 22.

Modric, mwenye umri wa miaka 25, bado hajawasilisha ombi rasmi la kutaka kuondoka uwanja wa White Hart Lane, lakini inaelekea angelipenda kuendelea kucheza soka mjini London.

"Ningelipenda kwenda Chelsea," alielezea, "lakini ningelipenda kuwaacha Spurs kama marafiki".