Ufaransa yaiondoa England robo fainali

Katika Robo fainali ya Kombe la Dunia la wanawake nchini Ujerumani kati ya majirani England na Ufaransa ilibidi mikwaju ya peneti kuamua mshindi.

Katika dakika 90 za mchezo, England iliongoza kupitia bao la Jill Scott mnamo dakia ya 59 kipindi cha pili.

Dakika mbili kabla ya kipenga cha mwisho England ikisubiri sherehe, Elise Bussaglia wa Ufaransa akaishona England bao la kusawazisha.

Mpira ulipowekwa katika ya uwanja kwa mda wa kuamua mshindi, kipindi cha kwanza na cha pili vilifikia mwisho bila mshindi, hivyo uwamuzi ikawa utafutwe kwa matuta.

England iliweza kuokoa mkwaju wa kwanza wa Ufaransa na kufunga hadi nyota wa Timu hio Faye White kuuelekeza mpira nje.

England 3-4 France - FAYE WHITE AKAPOTEZA

England 3-4 France - LE SOMMER AKAFUNGA

England 3-3 France - RAFFERTY AKAKOSA

England 3-3 France - BOMPASTOR AKAFUNGA

England 3-2 France - STONEY AKAFUNGA

England 2-2 France - THINEY AKAFUNGA

England 2-1 France - CARNEY AKAFUNGA

England 1-1 France - BUSSAGLIA AKAFUNGA England 1-0 France - KELLY SMITH AKAFUNGA

England 0-0 France - ABILIY ALIKOSA KWANZA

Hivyo basi Ufaransa kwa ushindi wa 4-3 Ufaransa inapiga hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza kabisa.

Ufaransa sasa itacheza na mshindi wa pambano kati ya Brazil na Marekani kwa fursa ya kutinga fainali itakayofanyika tareh 17 mwezi huu julai.