Simba yapoteza alama muhimu-Tanzania

Ligi kuu ya premier nchini Tanzania inaendela kupamba moto huku miamba wa soka nchini humo wakiendelea kuzoa alama muhimu.

Haki miliki ya picha google images
Image caption Simba yatoka sare

Katika mechi zilizochezwa hapo jana Simba ilitoka sare ya kufungana mabao 3-3 na Toto Africa, Yanga ikaicharaza Villa kwa mabao 3-2.

Coastal Union iliadhibiwa mbele ya mashabiki wake baada ya kunyukwa bao 1-0 na Azam.

Ligi hiyo inaendelea hii leo na mechi moja. Kagera Sugar itaialika Oljoro katika uwanja wao wa nyumbani.