Tevez agoma kucheza Ujerumani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tevez na Roberto Mancini

Maneja wa klabu ya Manchester city ya Uingereza Roberto mancini, amesema kuwa anamtaka mchezaji Carlos Tevez "nje ya ya klubu hicho" . Hii ni baada ya mshambulizi huyo kukataa kucheza dhidi ya Bayern Munich katika mechi za Ubingwa wa Ulaya.

Kulikuwa kumesalia dakika 35 kabla ya kumalizika huku Man City wakiwa wamelemazwa kwa mabao 2-0 wakati Mancini alimtaka Tevez aingie uwanjani ili asaidie kuokoa jahazi la Man City. Tevez mwenye Umari wa Miaka 27 akakataa kutii amri.

Mancini alisema kuwa "nikipewa fursa , atakuwa nje.Mimi na yeye tumemalizana”.

Carlos Tevez kwa muda sasa Teves amekuwa akitishia kukihama klabu hicho kwa madai ya kutaka kuwa karibu na familia yake lakini hadi sasa hajafaulu.

Na msimu huu wa ligi ya uingereza ilipoanza Meneja Mancini alimpokonya Teves unahodha na kumkabidhi Viny Kompany wadhifa huo.

Lakini mambo hayakuanzia hapo, mapema Edin Dzeko alionyesha kutoridhika baada ya alipotolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Nigel de Jong . Hii ilikuwa ni katika dakika ya kumi baada ya kipindi cha pili kuanza.

Dzeko alionyesha kutoridhishwa na badiliko hilo kwa kumtikisia kichwa meneja wake Mancini

Katika mechi nyengine ya kombe hilo Manchester United nusura watolewe kamasi katika uwanja wao wa Old Trafford na timu ya Basel.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ashley Young aiokoa Man U

Man U waliokuwa wanaongoza kwa magoli mawili kwa sufuri katika kipindi cha kwanza ,waliona Basel wakikomboa magoli yote katika kipindi cha pili na halafu kuongeza goli la tatu.

Iliilazimu Man U kupigana kufa na kupona hadi dakika ya mwisho ilikukomboa goli hilo la tatu kupitia mchezaji Ashley Young

Kwengineko Real Madrid ilichuna Ajax Amsderdam ya uholanzi magoli 3-0.

Magoli hayo yalifungwa katika kipindi cha kwanza na Cristiano Ronaldo, Kaka and Karim Benzema .

Inter Milan ikiwa ugenini iliifunga CSK Moscow 3-2

Kwa upande mwingine Villareal ya uhispania waliabishwa katika uwanja wao wa nyumbani walipo dungwa 2-0 na Napili ya Italy.

Leo usiku itakuwa zamu ya Arsenal kuikaribisha Olympiakos huko Emirati huku mabingwa watetezi wa kombe hilo FC Barcelona wakisafiri kumenyana na Barisov na Velencia ikiwaalika Chelsea.