Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 21 Septemba, 2009 - Imetolewa 22:34 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Zuma akiri kutokubaliana na wafanyakazi
 

 
 
Bwana Zuma asisitiza umoja na mshikamano na shirikisho la wafanyakazi
Rais Jacob Zuma akihutubia mkutano wa Cosatu
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema suala la kutoafikiana linadumu baina ya chama tawala cha ANC na Shirikisho la wafanyakazi (Cosatu) moja ya mshirika wake mkubwa kisiasa.

Chama cha ANC hivi karibuni iliikasirisha Shirikisho la Wafanyakazi baada ya kupinga kuwepo shirikisho hilo jeshini na Bwana Zuma akazidi kukazia suala hilo katika hutuba yake alipozungumza katika mkutano mkuu wa Cosatu.

Lakini hata hivyo Rais Zuma alisisitiza kuwepu umoja na kusema chama cha ANC ni sawa na ''kanisa kubwa'' linaloweza kuafiki bila ya kusutwa.

Bwana Zuma alitegemea kwa kiasi kikubwa msaada wa Shirikisho la wafanyakazi limuunge mkono alipochaguliwa kuwa rais katika uchaguzi mkuu mapema mwaka huu.

Na Cosatu inaaminika ndyo shirikisho kubwa zaidi kati ya mashirikisho matatu ya wafanyakazi ya kitaifa nchini Afrika Kusini.

Bwana Zuma ameitisha mkutano mkubwa ili wazungumze namna ya kuondoa tofauti zao.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha