Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 30 Desemba, 2009 - Imetolewa 08:43 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Obama ataka majibu kuhusu usalama
 
Ashutumu vyombo vya usalama
Rais wa Marekani Barack Obama
Rais Barack Obama ametaka vyombo vya usalama vya marekani kueleza mara moja ni kwa nini habari kuhusu raia wa Nigeria aliyejaribu kulipua ndege ya marekani hazikutumiwa ipasavyo.

Bwana Obama amezipa idara za usalama hadi alhamisi tarehe 31, kueleza jinsi Umar Farouk Abdulmutallab alivyoruhusiwa kupanda ndege ya marekani wakati ambapo tahadhari ilikuwa imetolewa kumhusu.

Wazazi wa Umar walikuwa wametahadharisha ubalozi wa marekani nchini Nigeria kuhusu mwenendo wa mwana wao.

Obama ameshutumu idara hizo kwa uzembe ambao nusura ungesababisha maafa. Amesema kuwa iwapo habari kumhusu Umar zingetumiwa vilivyo na idara za usalama, raia huyo wa Nigeria hangeruhusiwa kusafiri.

Umar mwenye umri wa miaka 23 alikuwa amejaribu kulipua ndege ya Marekani iliyokuwa na abiria 300 mnamo tarehe 25 mwezi desemba.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha