Mgomo waikumba Ugiriki

Mgomo wa saa 24 umeanza nchini Ugiriki kupinga hatua za taifa hilo za kubana matumizi.

Huduma za ndege za boti za abiria zimefutwa, shule, ofisi za serikali na maeneo ya kitalii yamefungwa huku hospitali zikiwa na wafanyakazi wachache.

Watu wasiopungua 16,000 wamejiunga katika maandamanao hayo yaliyoandaliwa na vyama vikuu vya wafanyakazi mjini Athens.

Tume ya Ulaya inajadili njia za kuimarisha benki za Ulaya kuzikinga na janga la Ugiriki.

Wakati huohuo, katika taarifa yake ya hivi karibuni kuhusu uchumi wa Ulaya, Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeonya kuwa ukuaji wa uchumi uko hatarini na kuwa kuna uwezekano wa kutokea kwa mdororo wa kiuchumi mwakani.