Magharibi yakasirishwa na kura za veto

Mataifa ya Magharibi yamelalamikia kura za veto za Uchina na Urusi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika muswada wa kuishutumu hatua ya Syria ya kupambana na waandamanai wanaopinga serikali.

Ufaransa imesema ilikuwa ni "siku ya huzuni" kwa Syria, huku balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa akionesha "hasira".

Muswada huo ulikuwa umepunguzwa umuhimu wake ili kuepuka kura hizo za veto, kuzuia kutajwa moja kwa moja kwa vikwazo.

Wakati huohuo, televisheni ya Syria imeonesha picha za mwanamke ambaye shirika la Amnesty International lilisema amekufa.