Berlusconi kupigiwa kura ya kukosa imani

Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi anakabiliwa na kura ya kukosa imani naye ndani ya bunge, kuhusiana na jinsi alivyoshughulikia kasfa za kiuchumi na masuala yake binafsi.

Bw Berlusconi anatarajiwa kutoathirika na kura hiyo, ingawa kwa kura chache.

Uwezo wa ulipaji madeni wa serikali ya Italia ulishushwa kiwango hivi karibuni na bunge kushindwa kuunga mkono sehemu muhimu ya bajeti wiki hii, na hivyo kusababisha kura hiyo ya kukosa imani.

Bw Berlusconi pia anakabiliwa na kesi ya ngono, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.