Liam Fox ajiuzulu

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Liam Fox, amejiuzulu baada ya siku kadhaa za tetesi kuhusu uhusiano wake na mmoja wa washauri wake (Adam Werrity).

Katika barua yake ya kujiuzulu Bw Liam Fox amesema kuwa alikosea aliporuhusu masuala yake ya binafsi yaingiliane na majukumu yake ya Uwaziri.