Uchaguzi Liberia kwenda duru ya pili

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais nchini Liberia unaonesha rais Ellen Johnson Sirleaf anayetetea kiti chake na mpinzani wake wakaenda raundi ya pili.

Bi Sirleaf amepta asilimia 44.5 ya kura, wakati mpinzani wake Winston Tubman akipata asilimia 26.5, imesema tume ya uchaguzi.

Katika nafasi ya tatu, muasi wa zamani Prince Johnson amepata asilimia 13.5, nafasi ambayo huenda ikamfanya mtu muhimu katika kugawanya kura.

Huu ni uchaguzi wa pili wa urais nchini Liberia, tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003.