al-Qaeda yatoa msaada Somalia

Mtu mmoja anayedai kuwa anatoka kundi la al-Qaeda amesambaza chakula cha msaada nchini Somalia, na kuashiria kuhusika kwa kundi hilo na wapiganaji wa al-Shabaab.

Mtu huyo aliyetambuliwa kuwa ni raia wa Marekani, Abu Abdulla Almuhajir, na akizungunza kwa lafudhi ya Kimarekani, aligawa chakula, hijab na Koran kwa watu waliopo katika kambi karibu na mji mkuu, Mogadishu.

Inadhaniwa kuwa huu ni mgao wa kwanza wa msaada wa al-Qaeda nchini Somalia ambayo imekumbwa na ukame.

Al-Shabaab imekataza mashirika ya misaada kufikia maeneo inayodhibiti.

Al-Shabaab inasema baadhi ya mashirika ya kimataifa yana ajenda ya kisiasa na wamekuza kiwango cha tatizo lililopo.