IMF latabiri kukua kwa uchumi Afrika

Shirika la Fedha Duniani IMF linatabiri kukua kwa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara kutaongezeka mwakani kwa asilimia sita kasoro.

Shirika hilo limesema ukuaji huo ni kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa, huku Afrika ikiuza vifaa vya viwandani ikiwemo mafuta na bati nchi za nje.

Hata hivyo IMF limeonya ukuaji wa uchumi kwa kasi ndogo katika nchi zenye uwezo zaidi itakuwa changamoto, huku nchi zenye uchumi ambao umeimarika zaidi kimataifa utaathirika zaidi, hasa Afrika Kusini.

Limeongeza kwamba licha ya kukua kwa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara, kuongezeka kwa bei za vyakula na mafuta kumebana bajeti za watu maskini na kuongeza mfumuko wa bei.