Msichana aliyetekwa nyara aachiliwa.

Msichana mwenye umri wa miaka 10 aliyetekwa nyara mwezi uliopita nchini Colombia na kushtua taifa nzima ameachiliwa huru.

Rais Juan Manuel Santos amesema kuwa Nohora Valentina Munoz aliachiliwa huru baada ya mashauriano ya upatanishi na shirika la kimataifa la msalaba mwekundu.

Bado haifahamiki nani alimteka nyara msichana huyo wakati alipokuwa akienda shule katika mji mdogo karibu na mpaka wa Colombia na Venezuela.

Lakini kundi la waasi la mrengo wa kushoto katika eneo hilo linashukiwa kutekeleza utekaji nyara huo.

Maelfu ya wanajeshi na maafisa wa polisi walihusika katika juhudi za kumuokoa msichana huyo.