Mgomo wa saa 24 Ugiriki

Imearifiwa kuwa vikosi vya Uturuki vimeingia kaskazini mwa Iraq kufuata kundi la waasi wa Ki-Kurdi kufuatia mashambulizi ya vifaa vya kijeshi ambako askari 26 wa Uturuki waliuawa na wengine kujeruhiwa.

Habari zinasema kua wapiganaji wa kundi la PKK walishambulia Wilaya ya kusini ya Hakkari iliyo kusini mashariki mwa nchi karibu na mpaka wa Iraq. Rais Abdullah Gul alitishia kulipiza kisasi.

Mamiya ya waandamanaji wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Athens mwanzoni mwa mgomo wa saa 24 ambao umeisababishia shughuli za nchi nzima ya Ugiriki kukwama.

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ufaransa inasema kua raia wake aliyetekwa nyara na kundi la Kisomali nchini Kenya mwezi uliopita amefariki.