Daraja laporomoka na kuua watu India

Watu wasiopungua 32 wamekufa na wengine 132 kujeruhiwa baada ya daraja kuanguka katika shughuli moja ya kisiasa kwenye jimbo linalozalisha chai kwa wingi la Darjeeling.

Zaidi ya wanavijiji 150 walikuwa wamesimama juu ya daraja hilo kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa waasi siku ya Jumamosi usiku, wakati lilipoanguka.

Maafisa wanasema waathirika walianguka zaidi ya mita 21 na kudondokea ndani ya mto wenye kasi wa Rangeet Khola.

Jeshi, kikosi cha zima moto na polisi wamesaidia wakazi katika shughuli za uokozi.

Takriban watu 60 waliokolewa siku ya Jumamosi usiku, lakini taarifa zinasema siku ya Jumapili shughuli ililenga zaidi kutafuta watu katika maeneo ya chini ya mto huo.