Wakazi Bangkok wauhama mji

Maji ya mto mkubwa mjini Bangkok yameongezeka zaidi wakati wakazi wanaendelea kuuhama mji huo kabla mafuriko mengine kuja mwishoni mwa wiki.

Kulikuwa na msongamano barabarani wakati wakazi wakitumia siku tano za mapumziko kuuhama mji.

Maji ya mafuriko yanaendelea kujaa kuelekea wilaya za kaskazini mwa Bangkok lakini katikati ya ya mji ni kukavu.

Maafisa wameonya kuwa mawimbi makubwa yatakuwa siku ya Jumamosi yakiungana na kutiririka kwa maji katika maeneo ya wazi ya kati ambayo yanaweza kuongeza mafuriko zaidi..

Mvua kubwa za masika zimesababisha mafuriko nchini Thailanda tangu Julai. Zaidi ya watu 370 wamekufa na nchi kuathirika vibaya.