Mateka Somalia waomba kuachiliwa

Wanandoa wa Afrika Kusini waliotekwa nyara na maharamia wa Kisomali mwaka mmoja uliopita wameomba waachiliwe huru

Bruno Pelizzari, mwenye umri wa miaka 52, alikamatwa na mkewe Debbie Calitz, wa miaka 49, walipovamiwa kwenye boti

Mtu wa tatu alifanikiwa kutoroka lakini wanandoa hao wamekuwa wameshikiliwa nchini Somalia tangu wakati. Maharamia wanataka kikombozi cha dola 4 milioni (£2.5m) ili waachiliwe.

Katika mawasiliano ya simu yaliyorekodiwa Bw Pelizzari amemweleza dada yake Vera Hecht: "tunataka uhuru wetu."

Maneno yake yanaonekana kuielekea serikali ya Afrika Kusini lakini nchi hiyo ina sera ya kutolipa kikombozi.