Watu wafika bilioni 7 duniani

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Watu wafika bilioni 7 duniani

Idadi ya watu duniani inatarajiwa kufiki bilioni saba hii leo, kwa mujibu wa hesabu za Umoja wa Mataifa. Idadi ya watu duniani imeogezeka mara dufu katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita.

Umoja wa mataifa uliadhimisha siku ya ongezeko la watu duniani mara ya mwisho mwaka 1999 kwa kubaini mtoto aliyezaliwa Bosnia kama mtu wa bilioni sita duniani.

Lakini mara hii Umoja wa Mataifa umeamua kutobaini mtoto yeyote, na badala yake kuwataka watu kutafakari hatari za kujaa kwa watu duniani.

Ongezeko kubwa la watu lilishuhudiwa katika nchi za magharibi baada ya vita vikuu vya pili vya dunia na idadi hiyo imeendelea kushamiri katika nchi zinazoendelea ambako wanawake hawapati mafunzo juu ya mpango wa uzazi.