Waarabu wasubiri Assad kujibu lawama

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamaji wanaompinga Rais Assad

Muungano wa mataifa ya kiarabu umesema unasubiri jibu kutoka kwa Rais Assad wa Syria kuhusiana na dai la kutaka akome kushambulia waandamanaji wanaopinga serikali yake.

Muungano huo ulifanya mkutano na wajumbe wa Syria nchini Qatar hiyo jana jioni.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Qatar alisema mkutano huo uliafikia kuwa Syria ikomeshe mashambulizi dhidi ya waandamanaji.

Mkutano huo ulifanyika wakati Rais Assad akionya kuwa mataifa ya magharibi yakiingilia kati yatazua tetemeko kubwa mashariki ya kati.