Ureno watafuta uwekezaji Angola

Waziri mkuu wa Ureno anatembelea nchi yenye utajiri wa mafuta Angola, inayodhamiria kuimarisha uwekezaji katika nchi iliyokuwa koloni lake ambayo imekumbwa na msukosuko wa uchumi kwenye ukanda wa Ulaya.

Msaidizi wa Rais wa Angola Carlos Maria Feijo amesema mpango wa ubinafsihaji wa Ureno utajadiliwa.

Shirika la Fedha Duniani limeiamuru Ureno kuuza makampuni yao ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Uwekezaji wa Angola nchini Ureno umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni.