Daktari wa Michael Jackson hatojitetea

Dr Conrad Murray alimwambia jaji hatojitetea katika kesi inayohusu kifo cha Michael Jackson.

Alikana kuua bila kukusudia lakini anaweza kutumikia kifungo na kufutwa kwa kibali chake cha kutibu iwapo atakutwa na hatia.

Dr Murray alimwambia Jaji Michael Pastor kuwa amefanya uamuzi kwa "uhuru na uwazi", ripoti zilisema.

Uamuzi huo umetolewa baada ya upande wa utetezi kumwita shahidi wake wa mwisho, mtaalamu wa dawa ya usingizi Dr Paul White.

Hoja za mwisho kutoka pande zote mbili zitaanza siku ya Alhamisi.