Wachezaji wa Pakistan wakutwa na hatia

Wacheza kriketi wa Pakistan Salman Butt na Mohammed Asif wamekutwa na hatia ya kosa la kupanga matokeo, katika mahakama moja jijini London.

Nahodha wa zamani Butt,27, na mrusha mpira Asif, 28, walikutwa na hatia ya kupanga njama za kudanganya na kukubali kupokea rushwa.

Wawili hao walipanga kwa makusudi kutekeleza jambo hilo katika mchezo wa hadhi ya Test dhidi ya England, mwaka jana.

Mrusha mpira mwingine, Mohammed Amir, ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 wakati huo, alikiri mashtaka hayo kabla ya kesi.